Posts

Showing posts from September, 2017

Nimeathirika kisaikolojia baada ya kuachwa nimeapa siji kuolewa tena

Image
Nilikuwa na mpenzi wangu ambaye tulianza naye shule ya msingi darasa la tano, wakati huo ulikuwa utoto mwingi, endapo hatukuwahi kulala, lakini tuliahidiaana kwamba tutapendana na hatuta achana. Alinipenda kweli kweli na mimi nilimpenda kweli kweli, ila tulikuwa hatuchezeani. Nilimkubali katika ahadi zake, hadi wazazi wetu walijua kwamba mimi na yeye tutakuja kuwa mme na mke, miaka mingi ikapita, tuka maliza shule ya msingi na sekondari, bado mahusiano yalikuwepo na yalikuwa na nguvu. Migogoro ilianza pale ambapo matokeo ya kidato cha sita yalipotoka, yeye alichaguliwa maana ufalu wake ulikuwa mzuri, mimi sikuchaguliwa maana ufaulu wangu haukuwa vizuri. Yeye akaenda UDOM mimi nikabaki nyumbani, nikijua ndugu yangu baada ya kumaliza ahadi yetu itatimia, kila rikizo bado alionesha msimamo kwaajili yangu kwamba ananipenda na ataishi na mimi, alipofika mwaka wa mwisho wakati na mimi najiandaa kwamba sasa naenda kuolewa, huyo mme mtarajiwa. Siku hiyo nilienda kutembelea kwao, nik...