Posts

Showing posts from August, 2017

Sijasoma nimeolewa na msomi ila ananitesa na elimu yake

Image
Nilipo maliza form four matokeo yangu yalitoa vibaya hivyo nikaamua nirudie ili kutafuta credit, niliendelea na uvumilivu huo, nikalipa kila kitu kwaajili ya mtihani wangu, wakati naendelea na maandalizi nilipata mchumba akaniambia ndakuoa, kabla ya miezi miwili kwenda kwenye chumba cha mtihani nikaonekana nina ujauzito wa huyo mwanaume, kwa mila zetu za kichaga lazima ufukuzwe nyumbani, nikafukuzwa nyumbani nikaenda kwa huyo mwanaume, nikasahau kabisa elimu yangu, tukaanza maisha, yeye alikuwa amesoma na alikuwa anafanya kazi ya ufamasia. Nikajufungua mtoto wa kwanza kabla mtot huyo hajaacha kunyonya nikapata mimba mingine akiwa na miezi mitano, mume wangu akanishauri tuitoe hiyo mimba nikakataa sana sana, akanibembeleza maana nilikuwa naoogopa kufa wengine wanapotoa mimba wanafia hiyo hiyo, siku moja asubuhi niliamka vibaya mwili haukuwa vizuri sasa kwa kuwa yeye ni daktari akasema atanihudumia bila kujua dawa anazo tumia kunitibu kumbe ni dawa za kutolea mimba, ile mimba ikatoka, ...

Mwanzo wa ndoa yangu

Image
Mimi kabla sijaolewa nilijua upendo ambao upo kipindi cha uchumba utaendelea hadi kipindi cha ndoa, lakini nikaja kuwa na mshangao baada ya mme wangu kuingia ndani ya ndoa. Maisha yalibadilika na kila kitu kikaenda kusiko takiwa, mume wangu alinikuta nimejitunza nilipokuwa kwetu tabia zangu zilimvuta kunipenda. Siku moja nilikuta nina dalili za magonjwa ya zinaa, nilipo amka asubuhi niliwaza sana nikasema hivi haya magojwa yanatoka wapi mbona mimi nimejutunza, sikujua nikasema inawezekana magonjwa yaha kuna njia nyingine ambayo yanaambukizwa, lakini nilienda kwa mtu ambaye ni mzima nikamweleza kile ambacho kinatokea kwenye mwili wangu, Yule mtu mzima akaniambia kweli wewe bado ni mtoto katika ndoa, magonjwa ya zinaa yanasababishwa na kujaamiana. Ukiona magonjwa kama hayo yameingia ujue kuna mmoja kati yenu si mwaminifu, akaniambia kama siyo wewe basi mumeo anatoka nje ya ndoa, niliposikia hayo moyo wangu uliuma sana kwa uchungu, nikawaza nakusema mimi narudi kwetu, kama mwanam...