Nimeathirika kisaikolojia baada ya kuachwa nimeapa siji kuolewa tena
Nilikuwa na mpenzi wangu ambaye tulianza naye shule ya msingi darasa la tano, wakati huo ulikuwa utoto mwingi, endapo hatukuwahi kulala, lakini tuliahidiaana kwamba tutapendana na hatuta achana.
Alinipenda kweli kweli na mimi nilimpenda kweli kweli, ila tulikuwa hatuchezeani.
Nilimkubali katika ahadi zake, hadi wazazi wetu walijua kwamba mimi na yeye tutakuja kuwa mme na mke, miaka mingi ikapita, tuka maliza shule ya msingi na sekondari, bado mahusiano yalikuwepo na yalikuwa na nguvu.
Migogoro ilianza pale ambapo matokeo ya kidato cha sita yalipotoka, yeye alichaguliwa maana ufalu wake ulikuwa mzuri, mimi sikuchaguliwa maana ufaulu wangu haukuwa vizuri.
Yeye akaenda UDOM mimi nikabaki nyumbani, nikijua ndugu yangu baada ya kumaliza ahadi yetu itatimia, kila rikizo bado alionesha msimamo kwaajili yangu kwamba ananipenda na ataishi na mimi, alipofika mwaka wa mwisho wakati na mimi najiandaa kwamba sasa naenda kuolewa, huyo mme mtarajiwa. Siku hiyo nilienda kutembelea kwao, nikamkuta mama wa mwanamme, akaniambia za mtaani, nikamwambia njema akasema hivi bado unatarajia kuolewa na mwananetu nikasema ndiyo, akaniambia sasa mtaishije, wewe hujasoma yeye amesoma, nikamwambia mama mimi na mwanao tumetoka mbali sana.
Akaniambia kwanzia sasa umwache mwanangu, nikamwambia mama tangu lini umekuwa hivi akasema, hivi mtu kama wewe unaweza kuolewa na mwanangu, au unajipendekeza kwa mwanangu ili awe mmeo, nikamwambia mama sisi tunapendana nikaondoka.
Kumbe mawazo aliyo nayo mama ndiyo aliyo nayo na mtoto, kumbe huyo ambaye namtarajia kwamba atakuwa mme wangu, kumbe amekutana na wanawake wengine chuoni, nikampigia simu siku hiyo na kumweleza mama yake alichosema, yeye akanijibu bora mama kakwambia mapema maana hata mimi nilitaka nikwambie hicho hicho, aliposema hivyo nilikimbia kama vile mtu mwenye kichaa nikatamani nife, sikula, sikunywa wala sikulala mawazo usiku na mchana.
Baada ya siku kadhaa ikabidi nipige simu kwanini umenifanyia hivyo, akaniambia wewe si type yangu haufanani na mimi, nikamwambia kwanini kunitenda mambo kama hayo akaniambia wewe sahau tu kila kilicho na mwanzo hakikosi kuwa na mwisho.
Nikamwambia tumetoka mbali sana toka darasa la tano, ahadi zetu zilikuwa ni kwamba tuje tuoane akaniambia wakati ule ulikuwa kwangu ni utoto, ila sasa ni mtu mzima sihitaji kuwa na mtu kama wewe.
Nili umwa miezi mitatu, nikalazwa hospitalini wakasema anaumwa ugonjwa wa mshituko wa moyo, nikawa hospitalini hapo, madokta wakasema ugonjwa wake huyu unatakiwa umpate mtu anayempenda kwa dhati, ndipo atapona kirahisi, wazizi wangu walijaribu kumpigia yule mwanaume simu ili aje auokoe angalau uhai wangu, akawambia kuishi au kufa ni mipango ya Mungu, usidhani kama mimi nikija basi ataishi kama ni wa kufa atakufa na kama niwa kuishi ataishi, wazazi wangu walihuzunika sana juu ya majibu ya huyo kijana.
Sasa nimekuwa natatizo la kukataa wanaume, maana ninakidonda ambacho bado kinavuja maji, na maumivu makali, kila mwanaume namwona ni mwongo tu ipo siku atanigeuka na kuniacha nife peke yangu, sitamani tena kuolewa kila nikikumbuka pito hilo.
Nyumbani kwetu waliniwekea kikao kwamba hadi sasa unafikisha miaka 31 bado hufikilii kuolewa, nikawaambia wazazi wangu mapenzi ipo siku yatanifanya nife, hivyo sitaki kuwa na mpenzi wa aina yeyote

Comments
Post a Comment