Sijasoma nimeolewa na msomi ila ananitesa na elimu yake
Nilipo maliza form four matokeo yangu yalitoa vibaya hivyo nikaamua nirudie ili kutafuta credit, niliendelea na uvumilivu huo, nikalipa kila kitu kwaajili ya mtihani wangu, wakati naendelea na maandalizi nilipata mchumba akaniambia ndakuoa, kabla ya miezi miwili kwenda kwenye chumba cha mtihani nikaonekana nina ujauzito wa huyo mwanaume, kwa mila zetu za kichaga lazima ufukuzwe nyumbani, nikafukuzwa nyumbani nikaenda kwa huyo mwanaume, nikasahau kabisa elimu yangu, tukaanza maisha, yeye alikuwa amesoma na alikuwa anafanya kazi ya ufamasia.
Nikajufungua mtoto wa kwanza kabla mtot huyo hajaacha kunyonya nikapata mimba mingine akiwa na miezi mitano, mume wangu akanishauri tuitoe hiyo mimba nikakataa sana sana, akanibembeleza maana nilikuwa naoogopa kufa wengine wanapotoa mimba wanafia hiyo hiyo, siku moja asubuhi niliamka vibaya mwili haukuwa vizuri sasa kwa kuwa yeye ni daktari akasema atanihudumia bila kujua dawa anazo tumia kunitibu kumbe ni dawa za kutolea mimba, ile mimba ikatoka, hapo sikujua lolote nilijua ni magonjwa tu.
Bado mtoto huyo hajaacha kunyonya ana mwaka mmoja ikaingia mimba nyingine, hiyo mimba wakati imeingia mimi nilikuwa sijatambua ila yeye alikuwa ametambua, zile dalili zikaanza kuonekana, wakati mwingine tumbo lilikuwa linauma sana, nilipo mwuliza mume wangu akaniambia ni dalili za UTI kumbe ananidanganya, akasema ndakutibu, aliporudi kutoka kazini, akanipa dawa na akanichoma sindano akaniambia hizi tiba ni kwaajili ya UTI baadaye nikakuta tumbo linaniuma sana nikimwambia anasema vumilia kunywa dawa litaacha kuuma.
Baadaye uchafu ukaanza kutoka sehemu za siri, akirudi kutoka kazini ananisafisha lakini ile hali ilizidi kila siku, wakati mwingine nikimwambia anakuwa mkali, tumbo linaendelea kuniuma, mimi najua kweli hii ni UTI.
Nilipoona hali yangu inazidi kuwa mbaya ikabidi niende nyumbani nikawaeleze wazazi, Baba yangu ni dactari wa siku nyingi, baada ya kumweleza akaniambia mwanangu UTI haiwezi kukufanya uchafu utoke kwa kiwango kikubwa kama hiki, akachukua vipimo vya mkojo wangu akaaja kugundua kwamba hiyo ni mimba.
Baba akaniambia mme wako alikuwa anakutoa mimba, niliposikia hayo nilichanganyikiwa nikajiuliza kwanini hakunishirikisha kwa kitu cha hatari kama hiki, nikasema mwanaume huyu si wakuishi naye maana io siku atakuja kuniua sasa, baadaye aliporudi akasema mbele ya wazazi yeye alikuwa hajui kitu akidai alikuwa anatibu UTI lakini ukweli ni kwamba ailikuwa anajua kila kitu.
Kumbe usipo soma ukaolewa na msomi si heshima kwa binti, maana kuna vitu atakuwa anakuficha kwasababu ya ujinga wako.
Unaposoma blogg hii nenda kwenye sehemu ya comment ukijibu swali hili je msomia aoane na msomi mwenzie na asiyesoma kwa asiye soma au kuwe na mchanganyioko

ilitakiwa msomi kwa msomi
ReplyDelete