Mwanzo wa ndoa yangu

Mimi kabla sijaolewa nilijua upendo ambao upo kipindi cha uchumba utaendelea hadi kipindi cha ndoa, lakini nikaja kuwa na mshangao baada ya mme wangu kuingia ndani ya ndoa.
Maisha yalibadilika na kila kitu kikaenda kusiko takiwa, mume wangu alinikuta nimejitunza nilipokuwa kwetu tabia zangu zilimvuta kunipenda.



Siku moja nilikuta nina dalili za magonjwa ya zinaa, nilipo amka asubuhi niliwaza sana nikasema hivi haya magojwa yanatoka wapi mbona mimi nimejutunza, sikujua nikasema inawezekana magonjwa yaha kuna njia nyingine ambayo yanaambukizwa, lakini nilienda kwa mtu ambaye ni mzima nikamweleza kile ambacho kinatokea kwenye mwili wangu, Yule mtu mzima akaniambia kweli wewe bado ni mtoto katika ndoa, magonjwa ya zinaa yanasababishwa na kujaamiana.

Ukiona magonjwa kama hayo yameingia ujue kuna mmoja kati yenu si mwaminifu, akaniambia kama siyo wewe basi mumeo anatoka nje ya ndoa, niliposikia hayo moyo wangu uliuma sana kwa uchungu, nikawaza nakusema mimi narudi kwetu, kama mwaname huyu ameanza kufanya hivi, huyo mtu akaniambia tulia usikuruuke fanya uchunguzi juu ya mume wako, basi baadaye nika mwuliza mume wangu inakuwaje magonjwa ya zinaa haya ambayo nipo nayo.

Mme wangu akaniambia mimi sijui yanatoka wapi kwa ukali kabisa kama vile hajui chochote, niakalia sana nakumwambia hujui chochote na huku unawanawake wengine wa nje, akaniambia kama umechoka uende nyumbani wala usilelete matatizo kwenye nyumba yangu. Nikamwambia mbona saizi umebadilika kwenye kipindi cha uchumba hakuwa hivyo akaniambia uliokuwa kwenu, nilikuwa nafanya juu chini nikupate, lakini saizi nimeshakupata sasa saizi nikutafute tena.

Aliponijibu hivyo ikawa kama mtu amelipasua jipu ambalo bado halija iva kwa maumivu makali, nikachukua nguo zangu niaondoa usiku huo huo.

Je wewe msomaji wa blog hii unanishauri nini

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Sijasoma nimeolewa na msomi ila ananitesa na elimu yake

Nimeathirika kisaikolojia baada ya kuachwa nimeapa siji kuolewa tena